Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAZIRI JAFO AFURAHISHWA NA UBUNIFU MKUBWA MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 2, 2025

2 JULAI  2025.


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameridhika na ubunifu wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 ambayo kimsingi yanaratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), vitu alivyovutiwa nanyo ni pamoja mpangilio bora wa mabanda kwa waoneshaji, idadi kubwa ya washiriki kwa mwaka wa maonesho 2025, miundombinu, kuwepo kwa usafiri maalum ndani ya Viwanja vya Maonesho unaoratibiwa na Posta. Aidha Waziri Jafo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi ili waweze kujifunza, kuona na kununua bidhaa na huduma zinazotolewa na Watanzania kwa Maendeleo endelevu, ameainisha hayo katika ziara yake ya matembezi alioifanya leo siku ya 5 ya Maonesho ya Sabasaba 2025 msimu wa 49.