WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA TANTRADE WAPATA SEMINA YA UONGOZI
- October 20, 2023

Tarehe 20 Oktoba, 2023.
DAR ES SALAAM
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wamepata semina ya Uongozi iliyotolewa na Taasisi ya Uongozi Institute kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 19 - 20 Oktoba, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa TanTrade Jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo ya siku mbili ilihusisha mada zikiwemo Uendeshaji wa Shirika na Uongozi Bora, Kufikia Ufanisi wa Bodi, Usimamizi wa Vihatarishi na Msingi wa Udhibiti wa Ndani pamoja na Usimamizi wa Fedha.
Akiongea katika Kufungua rasmi semina hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TanTrade, Prof. Ulingeta Obadia Mbamba alieleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wajumbe wa Bodi ambapo yanatarijiwa kuongeza Ufanisi zaidi kwenye Utendaji wa Bodi na kuongeza tija kwenye utekelezaji na Usimamizi wa majukumu waliyonayo kama Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka.