MASANJA MKANDAMIZAJI YUPO SABASABA.
- July 5, 2025

5 JULAI 2025.
Mchekeshaji nguli kutoka Tanzania ndugu, Masanja Mkandamizaji amefika kwenye kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere maarufu SABASABA grounds, kwa lengo la kujionea kwa macho bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini pamoja na zile zakigeni. Ikiwa ni siku ya nane ya Maonesho Watanzania kutoka mikoa yote mnakaribishwa Sabasaba kushuhudia Maonesho makubwa zaidi ya Afrika Mashariki yanayowakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali, Maonesho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania".