MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA 2025.
- July 10, 2025

9 JULAI, 2025.
Mke wa aliyekua Rais wa awamu tano hayati J.P.Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam SABASABA 2025 na kuzuru mabanda yanayoratibiwa na taasisi mbalimbali za umma kwa lengo la kujionea huduma na bidhaa zinazotolewa katika Maonesho ya Sabasaba 2025. Aidha mama Janeth Magufuli alipata wasaa wa kutembelea banda la Zanzibar na kuvutiwa na bidhaa za viungo, manukato, sabuni za mwani nk. Maonesho ya Sabasaba yameanza tarehe 28 Juni na kutamatika Julai 13 2025, Maonesho ya Sabasaba yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania".