Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

NEMBO YA MADE IN TANZANIA YAPATA MWITIKIO MKUBWA MAONESHO YA NANENANE ZANZIBAR

  • August 8, 2025

6 AGOSTI, 2025
ZANZIBAR.


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanaTrade) yaendelea kuendeleza bidhaa na huduma za Kitanzania kwa kuwafungulia fursa wazalishaji wa bidhaa za Kitanzania katika Maonesho ya Kilimo ya NaneNane katika banda la Made In Tanzania ambayo yanafanyika katika viwanja vya Dole Kizimbani, Zanzibar.

Aidha bidhaa za Kitanzania ambazo zinaoneshwa katika banda hilo ni Bidhaa za Asali kutoka Barefoot College Zanzibar, Mahnjumati Spices and Herbs kutoka Zanzibar, Refasha wauzaji wa bidhaa za Mwani kutoka Zanzibar pamoja na ZSTC kutokea Zanzibar.


Tembelea leo katika Banda la Made in Tanzania katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo NaneNane Dole Kizimbani Zanzibar.