Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2025

Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura

Uchaguzi 2025

NEMBO YA MADE IN TANZANIA YAVUTIA WAFANYABIASHARA, MAONESHO YA NANENANE DODOMA.

  • August 7, 2025

6 Agosti 2025
Dodoma.


Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade katika kutekeleza moja ya jukumu lake la kufahamisha na kuhabarisha Umma wa Tanzania kuhusu faida za kutumia chapa ya taifa ya "Made in Tanzania " kwenye bidhaa na huduma zinazozaliswa nyumbani Tanzania imekua kivutio kikubwa kwa wafanyabiashara wa sekta ya Kilimo ambao wamefika kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane 2025, Maonesho hayo yameanza tarehe 1 Agosti na kutamatika tarehe 8 Agosti 2025. Maonesho ya Nanenane yamebeba kauli mbiu inayosema "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025", Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika Jijini Dodoma.