Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

UBUNIFU WA MADE IN TANZANIA KUWASAIDIA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA UCHUMI WA BULUU ZANZIBAR.

  • January 8, 2026

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Tanzania, Bw. Hamis L. Lwembe, leo ametembelea banda la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) katika Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yanayofanyika kwenye uwanja wa Dimani, Fumba.

Katika ziara hiyo, Bw. Lwembe ameipongeza TanTrade kwa juhudi kubwa inazozifanya katika kuwawezesha wafanyabiashara wa ndani kupenya katika masoko ya kikanda na kimataifa, kupitia ubunifu wa nembo ya Made in Tanzania.  

Amesema kuwa ubunifu huo si tu kwamba unatangaza bidhaa za Tanzania nje ya nchi, bali pia unatoa heshima kwa wazalishaji wa ndani na kuwajengea imani ya kibiashara. Aidha, ameahidi ushirikiano kati ya chama cha wafanyabiashara na TanTrade ili kuhakikisha wafanyabiashara wengi zaidi wananufaika na fursa hizo.