MADE -IN-TANZANIA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA NISHATI- DAR ES SALAAM
- October 13, 2025

Leo tarehe 10 Oktoba 2025, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) imeratibu Makampuni ya Excel.... Waandaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Nishati "Solar and Energy Expo" yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Aidha, pamoja na uratibu huo kwa mujibu wa taratibu, TanTrade inaendelea kuhamasisha usajili wa wazalishaji na Masoko ya bidhaa 'Made in Tanzania' kwa kuonesha sampuli ya vifaa vya umeme ikiwemo nyaya,transfoma na Mita zinazozalishwa nchini na kampuni ya AFRICAB.
Elimu ya alama rasmi ya Bidhaa za Tanzania "Made in Tanzania, Fahari ya Tanzania" inaendelea kutolewa na kuhamasisha kutumia bidhaa za ndani na kujenga Uchumi wa Tanzania. Watembeleaji wamempongeza Mkurugenzi wa TanTrade na Timu yake kwa juhudi kubwa anazozifanya za kuendelea kuzitangaza bidhaa za Tanzania. "Made in Tanzania, Fahari ya Tanzania".