Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

LINGHANG GROUP YAIPA TANTRADE OFISI YA KUHAMASISHA 48 DITF SHANGHAI

  • November 10, 2023

Tarehe 8 Novemba, 2023
SHANGHAI, CHINA

Mamlaka ya Maendeleo Biashara Tanzania (TanTrade) imefanya kikao na kampuni ya LINGHANG Group ya China kujadili fursa mbalimbali za Biashara na Uwekezaji China na Tanzania.

Katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TANTRADE aliwaeleza wawekezaji hao kutoka China kuwa kuna maeneo mengi ya kimkakati ambayo kampuni hiyo inaweza faidika nayo nchini Tanzania.

Aidha, Bw. Mhambe pia aliwakaribisha wawekezaji hao katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (Sabasaba) ambayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.

Aisha, kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa LINGHANG Group Ms. Lisa WANG alieleza kampuni zake zilivyojipanga kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha Uchumi kwa nchi za Maziwa Makuu.

Ms. Lisa Wang alitoa nafasi katika ofisi zake zilizopo katika Jimbo Shanghai, Guanzhou na Shandong kwa TANTRADE kutumia ofisi hizo katika kuhamisisha ushiriki wa majimbo zaidi ya China katika Maonesho yajayo SABASABA.

Pia, Ms. Lisa alitoa usafiri kwa Watumishi wa TANTRADE ambao watakuwa wakisafiri nchini China kuhamasisha makampuni mbalimbali ya China kushiriki Maonesho hayo akiamini ni dirisha litalotoa fursa nyingi za Uwekezaji na Biashara kati ya nchi hizo mbili na hivyo kupunguza utofauti wa Biashara kati ya China na Tanzania.