KUMEKUCHA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM (SABASABA) 2025
- May 6, 2025

6, MEI 2025
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kuangazia maswala mbalimbali ya kimaandalizi na uratibu wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2025 ambapo kwa sasa umebaki mwezi mmoja na wiki chache kufikia kuanza kwa maonesho hayo ambayo yataanza tarehe 28 Juni na kutamatika 13 Julai 2025. Maonesho hayo kwa mwaka huu yamekua na maboresho kadha wa kadha hususan kwenye eneo la kuhifadhi nafasi ambapo mchakato huo unafanyika kidigitali kupitia tovuti ya TanTrade, www.tradefair.tantrade.go.tz,
Kikao hiki kimefanyika leo katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.