KIKWETE ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA 2025.
- July 13, 2025

13 JULAI, 2025.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025, nakutembelea taasisi mbalimbali kama vile, Kilimo, Sido, Posta, Bunge, Chuo Kikuu cha Mlimani kwa lengo na kuona huduma na bidhaa wanazozitoa. Maonesho ya Sabasaba yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania. Maonesho haya yamekusanya washiriki kutoka mataifa mbalimbali kama vile, Egypt, Uganda, Kenya, Ghana, Congo, India, China, nk. Maonesho haya yanafanyika katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere Sabasaba Grounds barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.