Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

JAKIBUNI MSHIRIKI MAONESHO YA 49 YA DAR ES SALAAM (SABASABA)

  • January 14, 2025

Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Lucy Mbogoro akiwasilisha fursa za masoko na bidhaa zinazohitaji Uwekezajı zaidi nchini katika kongamano la Biashara na Uwekezajı baina ya Tanzania na Japani linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Johari Rotana iliyopo Dar es Salaam.

Bi. Lucy amechukua nafasi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa M Khamis kuwakaribisha wadau wa Biashara kutoka Japani kushiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yatakayoanza 28 Juni hadi 13 Julai 2025 na pia kuwakaribisha katika kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii litakalofanyika pembezoni mwa maonesho ya Expo 2025 Osaka Japan tar 26 Mei 2025