WAZIRI JAFO ATANGAZA BUNIFU TATU BORA ZA MADE IN TANZANIA
- February 11, 2025

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) ametangaza rasmi bunifu tatu bora zilizoshinda nembo ya Made in Tanzania katika hafla iliyofanyika leo tarehe 11 Februari, 2025 katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.
Aidha Mhe. Jafo ameiagiza Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuhakikisha kuwa mchakato “Made in Tanzania “ unakamilika haraka ili iweze kuzinduliwa katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam , kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa na nembo yake katika bidhaa kwaajili ya kutangaza bidhaa zote za nchi katika masoko mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuongeza ushindani.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bi. Latifa khamis amesema kuwa ni muhimu kuwa na nembo ya “Made in Tanzania “ ambayo itakuwa ikitambulisha bidhaa na huduma za Tanzania na itawezesha bidhaa za Tanzania kupata haki ya ubora.