Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

India kuimarisha uhusiano wa biashara na Tanzania

  • July 25, 2024

Kaimu Mkurugenzi wa  Usimamizi wa Biashara Bw. Crispin Luanda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE amepokea wafanyabiashara kutoka India walioongozwa na  Bw. Kunal Singhal ambaye ni Mkurugenzi wa “Eazy ERP Technologies “ ambapo ameeleza kuwa wamekuja Tanzania kutafuta fursa za uwekezaji katika Sekta ya Kilimo, Uchimbaji wa Madini , Mafuta, Madawa, Fedha, Usafirishaji , Vipuri na Teknolojia mbalimbali , wakati walipotembelea ofisi za TanTrade zilizopo barabara ya Kilwa, JIjini Dar es Salaam leo tarehe 24 Julai, 2024.

Aidha Bw. Luanda amewaeleza kuwa TanTrade itaendelea kutoa ushikiano kwa wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na masoko ili pande zote mbili ziweze kunufaika.