KUMEKUCHAA SABASABA ZOO YAFUNGULIWA RASMI KWA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA.
- December 26, 2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbasi ametembelea Makao Makuu ya TanTrade na kuonana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Dkt. Latifa Mohamed Khamis, ikiwa ni sehemu ya kujionea Sabasaba Zoo ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Wananchi wa Dar es Salaam na Mikoa ya Jirani Kuja kutembelea viwanja vya Mwl J.K.Nyerere (Sabasaba) Kujionea wanyama mbalimbali na kupata fursa ya kumlisha Tembo.
Aidha amebainisha kuwa wanyama watakuepo msimu wote wa sikukuu za Krismass na Mwaka Mpya na wataendelea kuwepo hadi tarehe 5 Januari, 2026.