Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAMILIKI WA VIWANDA WAPATA ELIMU YA MITAJI WEZESHI KATIKA TAASISI ZA FEDHA

  • September 27, 2024

Dar es salaam
27/09/2024

Maonesho ya Kimataifa ya Viwanda  (TIMEXPO) 2024 yanaendelea ambapo Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na  Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania(CTI) wameenda mdahalo maalumu  kwaajili ya utoaji wa elimu ya mitaji na mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ili waweze kujiendeleza katika shughuli zao za uzalishaji wa bidhaa viwandani ulionafanyika leo tarehe 27 Septemba, 2024
 katika ukumbi wa Mhe. Ali Hassan Mwinyi ulipo Kiwanja cha JK. Nyerere (Sabasaba) barabara ya Kilwa Jijini Dar es salam.

Aidha  Mdahalo huo watoa mada mbalimbali kutoka katika taasisi za kifedha zikiwemo StanBic Bank, NEEC, TAPAIA, TIB, CRDB, TanTel Holding wametoa elimu juu ya kupata mikopo kutoka benki na kuweza kujiendeleza katika uzalishaji wa bidha zao.