Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAONESHO YA VIWANDA 2024, YAWAINUA WAJASILIAMALI

  • September 27, 2024

Ikiwa ni muendelezo wa siku ya pili ya Maonesho ya Wazalishaji Tanzania, Mwenyekiti wa Kituo cha Uwekezajı Tanzania (T.I.C)  Dr Binilith Mahenge ametembelea  maonesho ya pili ya Kimataifa ya Viwanda TIMEXPO 2024, ambayo yameratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kwa kushirikiana na Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI).


Dr Mahenge  amepongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Kwa kuandaa maonesho haya kwani wamekua mkombozi Kwa wazalishaji Wakitanzania hususan wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa, leo tarehe 27 Septemba, 2024 , katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere, barabara ya Kilwa, maarufu kama Sabasaba, vilivyopo barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam