Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA NA BIASHARA YAFUNGULIWA RASMI

  • May 22, 2024

21 Mei, 2024
Dodoma.

Maonesho ya wiki ya Viwanda na Biashara yaliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na TanTrade yamezimduliwa rasmi leo.

Maonesho haya ambayo yanafanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma yamefanyika sambamba na usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara yamefunguliwa Rasmi na Mhe. Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mhe. Omar ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa maandalizi mazuri ya Maonesho hayo na kuahidi kushirikiana na TanTrade katika kuandaa Maonesho kama haya Zanzibar wakati wa usomwaji wa bajeti ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ili kutoa fursa kwa waheshimiwa wabunge na wadau kufahamu kazi na majukumu yanayotekelezwa na Serikali kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Mgeni rasmi alitoa rai kwa waheshimiwa wabunge kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaowawakilisha kuwa na desturi ya kupenda kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili kukuza viwanda hivyo na uchumi wa nchi. Maonesho haya yatahitimishwa rasmi tarehe 22 Mei, 2024