Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

INDIA YAPANGA KUSHIRIKI MAONYESHO YA 47 YA DITF (Sabasaba) KWA MAFANIKIO.

  • July 21, 2023

...................................
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
3 Mei, 2023.


Ubalozi wa India nchini Tanzania umeendelea na maandalizi ya kuratibu Washiriki kutoka India kwa ajili ya Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yatakayoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 ambapo mpaka sasa makampuni 35 kutoka Jimbo la Haryana yamethibitisha kushiriki.
Hayo yameelezwa na  Balozi wa India nchini Tanzania Mheshimiwa Narender Kumar alipotembelea Ofisi za TanTrade katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K Nyerere (SabaSaba) tarehe 3 Mei 2023 kwa madhumuni ya kuendelea na maandalizi ya ushiriki wa India katika Maonesho hayo.

Bw.Narender amesema kampuni hizo pia zitapenda kupata washirika wa kibiashara katika sekta za uvuvi, kilimo, madini, afya, elimu na miundo mbinu.

Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Biashara TanTrade Bw.Fortunatus Mhambe  ameushukuru Ubalozi wa India nchini Tanzania na kusema kuwa TanTrade imejipanga na iko tayari kuwahudumia wanachama wa makampuni hayo, pia itaendelea na uratibu ili kuhakikisha ushiriki wao unakuwa na tija.