UTAMBULISHO WA MRADI WA KUENDELEZA UWANJA WA MAONESHO WA MWL. JULIUS NYERERE
- June 17, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis amezungumza na Waandishi wa Habari na kueleza mpango wa Tantrade kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kujenga uwanja wa kisasa wa Maonesho wenye hadhi ya Kimataifa, unaoendana ma hali iliyopo ya kimaendeleo duniani. Maboresho ya Uwanja huu yatahusisha kumbi za kisasa za mikutano na shughuli mbalimbali, kama maegesho ya kisasa ya magari, maeneo ya michezo ya watoto, vituo vya biashara, ofisi za kisasa, migahawa pamoja na hoteli. Bi. Latifa amewakaribisha wawezekaji wenye uwezo wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa hii yenye maslahi mapana kwa taifa.
Akiongea katika mkutano huo wa waandishi wa habari, Ndugu. David Kafulila, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP) ameipongeza TanTrade kwa kutekeleza azma ya ushirika kati ya Serikali na Sekta Binafsi kwenye kufanikisha maendeleo