MHE. NAIBU WAZIRI MKUU AZINDUA SERA YA TAIFA YA BIASHARA
- July 30, 2024

Dar es salaam,
30 Julai 2024.
Mhe. Dkt Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amezindua Sera ya Taifa ya Biashara ambayo imelenga kuboresha mazingira ya Biashara ili kuendana na Mpango Mkakati wa Dira ya Taifa na kuleta Ukuaji wa Uchumi wenye Tija.
Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Biteko ameeleza kuwa Sera hii imelenga kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanakuwa na uwanda mpana wa kufanya biashara zao kiushindani na kuweza kushiriki vizuri katika kufanya biashara katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Hivyo anategemea Sera hii itaongeza Ushindani wa mauzo nje ya nchi na kuongeza wigo wa bidhaa kufikia masoko mapya.
Mhe. Biteko amemalizia kwa kutoa wito kwa Sekta zote za Serikali ambazo zinazalisha na kufanya kazi na wafanyabisahara kusoma Sera hii na kuisimamia ipasavyo.
Aidha, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo amesisitiza kuwa Sera hii mpya ambayo inaakisi hali na mazingira ya sasa, pia iwe chachu kwa wafanyabiashara wote kuchukua fursa na kufanya biashara kidijitali ili kufikia masoko mengi zaidi.
TanTrade imeshiriki kwenye uzinduzi huo kama taasisi yenye Mamlaka katika kusimamia Maendeleo ya Biashara nchini Tanzania.