Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WAKUU WA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA ZANZIBAR KUSAJILI JUKWAA LA WAKURUGENZI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA.

  • March 13, 2025

3, Machi 2025.

Jukwaa la Wakuu wa Taasisi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kutoka Tanzania bara limekutana na Wajumbe kutoka Taasisi za Umma Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya utaratibu wa kusajili, kuendesha na kuratibu Jukwaa la Wakuu wa Taasi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kwa upande wa Zanzibar, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ya kuundwa kwa jukwaa hilo kwa lengo la kutatua kero mbalimbali za wananchi pamoja na kero za Muungano katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Wakuu wa Taasisi kilichofanyika Zanzibar mwezi Januari 2025.

Aidha Ujumbe wa Zanzibar umeongozwa na Msajili wa Hazina (TR) Ndg. Abdullwahid Ibrahim Sanya na kwa upande wa Jukwaa la wakuu wa Taasisi Tanzania Bara uliongozwa na Katibu Mtendaji, Ndg. Abdulrazak Badru ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF akimwakilisha Bi. Latifa Khamis Mkurugenzi Mkuu TanTrade na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasi za Umma kutoka Tanzania Bara.

Akiongea katika kikao hicho Ndg. Badru ameainisha faida mbalimbali zitakazopatikana kwenye jukwaa linalotarajiwa kuanzishwa na namna ambavyo zinaenda kuboresha utendaji kazi wa taasisi wanazosimamia.