HALMASHAURI YA GAIRO NA TANTRADE YAJADILI UENDELEZAJI WA SOKO LA UKWAMANI
- December 4, 2023

4 Desemba, 2023
Dar es salaam
Menejimenti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade) imekutana na Ujumbe wa Halmashauri ya Gairo ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Sharifa Ramadhan ili kujadili namna bora ya kuendeleza Soko la Ukwamani Gairo kwa kulifanya la Kisasa na lenye uwezo wa kuhudumia maeneo mengi ndani na nje ya nchi.
Soko la Ukwamani- Gairo lipo Kimkakati kuongeza thamani kwa mazao mbalimbali yanayozalishwa ndani na nje ya Mkoa wa Morogoro kama vile mahindi, mpunga, maharage na mengineo kutoka Wilaya mbalimbali.
Wafanyabiashara na Wananchi wa Gairo na maeneo ya jirani wataendelea kuwa wanufaika wakubwa wa soko hilo kwani litahudumia Jiji la Dodoma, Dar es salaam, Arusha na hata nje ya nchi kwa mazao ya nafaka yaliyoongezwa thamani.
Menejimenti ya TanTrade imewaalika wafanyabiashara pamoja na uongozi wa Gairo kuendelea kutangaza fursa kupitia majukwaa mbalimbali yanayoandaliwa kitaifa na Kimataifa ikiwemo Expo2023 Doha, Qatar na Maonesho ya Sabasaba- 48DITF 2024 ili kuongeza mzunguko wa Biashara na kukua zaidi.