Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

ETHIOPIA YAJIFUNZA UENDESHAJI NA UKUZAJI BIASHARA KUTOKA TANTRADE

  • April 6, 2025

___
04 Aprili, 2025
Dar es Salaam.

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imepokea ujumbe kutoka ubalozi wa Ethiopia nchini Tanzania ukiongozwa na Mhe. Abdulkarim Mulu  Naibu Waziri wa Biashara na Uunganishaji wa Kikanda wa Ethiopia “State Minister of Trade and Regional Integration of Ethiopia” ambao umejadili maswala mbalimbali ya namna ya ukuzaji na uendelezaji biashara nchini kwao, kikao kilichofanyika katika ofisi za TanTrade, zilizopo kiwanja cha Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.


Wakizungumza na TanTrade ujumbe huo umeipongeza TanTrade kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya upande wa biashara na kuhitaji kufahamu njia ambazo wanatumia iliwaweze kupata ujuzi wa namna bora uendelezaji biashara nchini kwao.