ETHIOPIA NA TANZANIA KUDUMISHA UHUSIANO WA BIASHARA.
- February 5, 2025

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imepokea ujumbe kutoka ubalozi wa Ethiopia ambao umekuja kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana katika nchi ya Ethiopia nakujua fursa ambazo zinapatikana katika nchi ya Tanzania, ujumbe huo umefika leo katika ofisi za TanTrade jijini Dar es salaam tarehe 04 Februari, 2025.
Ujumbe huo umeainisha fursa mbalimbali za masoko kwa bidhaa za Kitanzania pamoja na uwepo wa bidhaa za biashara kama bidhaa za Ngozi na Kahawa ambazo zinapatikana kwa wingi katika nchi ya Ethiopia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M. Khamis amepokea ujumbe huo nakuahidi kuwa taasisi itatoa ushirikiano ili kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara, nakuyataja baadhi ya Mazao ya Ethiopia kama Kahawa kuwa ni mazao abayo yamekuwa na ubora na mvuto zaidi sokoni na kuwakaribisha kuja kushiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam.