SIKU YA MAZINGIRA YATOA HAMASA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.
- July 6, 2025

6 JULAI, 2025.
Siku ya mazingira yanuwia kutoa hamasa kwa Watanzania kuendelea kutumia nishati safi kama vile gesi, umeme na makaa ya mawe ili kuiendeleza Tanzania kua kijani zaidi, Aidha wadau wa mazingira kutoka Tanzania na nchi nyingine wameshiriki sikuu hii ya mazingira ambayo imefanya siku ya 9 ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam SABASABA 2025, siku ya Mazingira imebeba kauli mbiu inayosema "Matumizi ya Nishati Safi na Uhifadhi wa Mazingira, kwa Ustawi Bora wa Tanzania". Siku ya Mazingira imefanyika katika Ukumbi wa Rashida Mfaume Kawawa (Dome) uliopo katika kiwanja cha Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam barabara ya Kilwa.