DKT. LATIFA ATOA KONGOLE KWA WASHIRIKI WA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA.
- September 22, 2025

Leo tarehe 20 Septemba 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Dkt. Latifa Khamis, akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigella, wametembelea baadhi ya mabanda ya waoneshaji katika Viwanja vya Samia yanapofanyika Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini.
Katika ziara hiyo, viongozi hao wamepata fursa ya kuzungumza na wajasiriamali na wadau mbalimbali wa sekta ya madini na viwanda vidogo vidogo waliopo kwenye mabanda hayo, wakijionea ubunifu, teknolojia, na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini. Dkt. Latifa amesisitiza umuhimu wa kutumia majukwaa kama haya kuhamasisha matumizi ya bidhaa za ndani na kuongeza ushiriki wa Watanzania kwenye masoko ya kikanda na Kimataifa.