Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2025

Kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura

Uchaguzi 2025

DKT. LATIFA AITANGAZA MADE IN TANZANIA KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA.

  • September 22, 2025

20 Sept 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Dkt. Latifa Mohamed Khamis,  ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa na watoa huduma nchini kuendelea kutumia Nembo ya Made in Tanzania kama chombo muhimu cha kutambulisha ubora wa bidhaa zao katika masoko ya kimataifa.

Akizungumza katika Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Samia, Geita,  Dkt. Latifa amesema kuwa nembo hiyo ni alama ya taifa inayosaidia kuongeza thamani ya bidhaa, kuaminika kwa wateja, na kusaidia bidhaa za Tanzania kushindana kwenye masoko ya kikanda na duniani kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Latifa amewakaribisha rasmi wazalishaji wote kushiriki kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba (DITF) yatakayofanyika mwakani katika viwanja vya Julius Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa hiyo ni fursa adhimu kwa wafanyabiashara kujitangaza, kupata mitanda