KAMATI KUU YA KITAIFA YA DITF YAKETI KUELEKEA MAONESHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA DAR ES SALAAM (SABASABA)
- April 24, 2025

23 Aprili, 2025.
Dar es Salaam.
Wajumbe wa kamati Kuu ya Kitaifa ya Maonesho ya Sabasaba wamekutana na kuangazia ni kwa jinsi gani wataboresha huduma na usimamizi kwa ujumla katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (49TH DITF) 2025 yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni na kutamatika 13 Julai, 2025.
Aidha Kamati Kuu hiyo inayohusisha wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi za pande zote mbili za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imenuwia kuboresha maonesho hayo na kuwa mazuri zaidi baada ya kufanya tathimini ya Maonesho ya mwaka Jana.
Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika Uwanja wa Mwl. J.K. Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam