Chato Utalli Festival
- November 29, 2023

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) tarehe 26 Novemba, 2023 imeshiriki sherehe za ufunguzi wa Tamasha la Utalii Chato Chato Utalli Festival ambalo limeandaliwa na Mkuu wa Wilaya akishirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Chato. Mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi alikuwa Mh. Abdalla Ulega (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye alishuhudia zoezi la utiaji saini MoU ya ushirikiano katika kutoa mafunzo ya Utalii kati ya VETA na Chuo cha Taifa cha Utalii na kukabidhi vyeti kwa vijana 476 waliohitimu mafunzo hayo na kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli. Aidha, katika hotuba yake pamoja na mambo mengine Mh. Mgeni rasmi alipongeza TanTrade kwa ushiriki wake katika kufanikisha maandalizi ya Tamasha hili.