Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA CHINA KUKUZA BIASHARA NA KUPAUA WIGO WA UWEKEZAJI TANZANIA

  • July 25, 2023


..............................
Na. Norah Thomas-TanTrade Dar es salaam.
4 Julai, 2023.

Waziri wa Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shaban Omary amesema ushirikiano baina ya Tanzania na China unasaidia kurahisisha ufanyaji wa biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili  na kupanua Masoko na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Waziri Shaban ameyasema hayo Julai 4, 2023 katika hafla ya  siku ya China (CHINA DAY) iliyofanyika kama programu moja wapo ya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (Sabasaba) yaliyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 katika Viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere Jijini Dares Salaam.

Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar zina historia ndefu ya ushirikiano ambao umestawi katika sekta mbalimbali, kuanzia teknolojia, miundombinu ya kilimo na utalii, Uhusiano huu wenye matunda ni ushuhuda na una dhamira  ya pamoja katika kukuza ukuaji wa uchumi na maendeleo.

‘’China mara kwa mara imekuwa mojawapo ya washirika wakuu wa biashara na Tanzania, na tumeshuhudia hilo kwa  matokeo chanya ya ushirikiano huu tunayoyaona katika uchumi wetu wa ndani, pia  uwekezaji wa China umeleta nafasi za kazi, miundombinu iliyoboreshwa, na kuendeleza ukuaji wa viwanda muhimu. Wachina wametusaidia katika kuunga mkono juhudi zetu za kuinua uchumi na kupunguza umaskini,  tunapoadhimisha Siku ya Uchina, tunatambua pia maendeleo ya ajabu yaliyofanywa na China nchini na kuifanya nchi yetu kuwa moja ya nchi yenye nguvu ya kiuchumi duniani’’ Alisema.

Aidha aliendelea kusema kuwa, Maendeleo ya haraka ya China, miundombinu ya kuvutia miradi, na kujitolea kwa uvumbuzi kumeifanya kuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengi, likiwemo Taifa letu.

‘’Tunaipongeza serikali ya China kwa kujitolea kwa maendeleo endelevu na juhudi zake kupunguza umaskini., Zaidi ya hayo mfumo wa FOCAC umefungua njia mpya za ushirikiano, kuunganisha mataifa na kukuza biashara kati ya mataifa. Tanzania ikiwa iko kimkakati katika bara la Afrika iko tayari kufaidika sana na mpango huu. Tunaamini kwamba FOCAC itachangia zaidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na kukuza biashara na uwekezaji kati zetu’’ aliongeza.

Pia Mhe. Waziri,  ameipongeza  serikali ya China na Tanzania kwa kudumisha ushirikiano huu wenye tija na kutoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya  Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba  pia  kutumia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya nchi na zile zilizopo nchini China.

Naye, Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Wachina ni washirika wakubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na maadhimisho haya ya Sabasaba na ujenzi wa eneo la biashara la Ubungo(Ubungo busterminal zamani) litakalo kuwa na Malls nyingi katika eneo hilo.

Naye Balozi wa Jamhuri ya China Bi. Chen Mingjian amesema maadhimisho hayo yameendeleza mahusiano mazuri yakibiashara na kitamaduni kati ya Tanzania na China na Africa.