Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

PONGEZI TANTRADE KWA KURATIBU VYEMA MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 13, 2025

13 JULAI, 2025.


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade kwa kuratibu vyema Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025. Ameipa TanTrade kongole yao kwa kuongeza idadi ya washiriki, matumizi ya teknolojia na ubunifu wa kuwepo kwa usafiri unaotumia nishati safi ndani ya Maonesho ya Sabasaba, ameainisha hayo katika siku ya ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam iliyofanyika katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.