Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

PONGEZI SANA TANTRADE KWA MAONESHO BORA YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA 2025.

  • July 16, 2025

15 JULAI, 2025.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis amepokea tuzo ya pongezi siku ya ufungaji wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 kwa kuandaa vyema Maonesho ya Sabasaba yaliyoanza tarehe 28 Juni na kutamatika Julai 13 2025. Maonesho ya Sabasaba yamekua suluhishi la masoko kwa bidhaa na huduma zinazozaliswa na Watanzania, lakini pia wajasiriamali wamepata fursa hadhimu ya kutangaza bidhaa na huduma zao kimataifa. Tuzo hiyo alipokea katika ukumbi wa Ali Hassan Mwinyi uliopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere maarufu (Sabasaba grounds) barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.