PONGEZI WATUMISHI WA TANTRADE, SABASABA 2025 IMEFANA.
- July 8, 2025

7 JULAI, 2025.
Watumishi wa TanTrade wamepokea kongole yao kutoka Kwa Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi kwa kufanya kazi ya uratibu kwa bidii na weledi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam SABASABA 2025. Moaneshi ya Sabasaba ya mwaka huu yamechukua sura mpya kwenye upande wa kuboresha mifumo ya ukataji tiketi, malipo ya maegesho ya magari pamoja na huifadhi wa nafasi Kwa waoneshaji mambo hayo yote yamefanyika kidijitali. Maonesho ya Sabasaba yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania".