Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

PONGEZI TANTRADE MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 4, 2025

3 JULAI, 2025


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kazi nzuri walioifanya ya kuratibu Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam SABASABA 2025. Mkuu wa Wilaya ametoa pongezi hizo wakati akifanya matembezi kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi sambamba na kuwatembelea wafanyabiashara mbalimbali wanao uza bidhaa na huduma katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. Maonesho ya Sabasaba yameanza tarehe 28 Juni na kutamatika 13 Julai 2025.