WAZIRI GAKOSSO WA KONGO AVUTIWA NA MAONESHO YA SABASABA 2025.
- July 8, 2025

8 JULAI, 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Jean Claude Gakosso ametembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Sabasaba 2025 nakuvutiwa na Banda la Zanzibar, Maliasiri na China, aidha Waziri Gakosso alipata nafasi ya kumtembelea Bi. Latifa M. Khamis Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade na kumpa pongezi kwa kuratibu vyema Maonesho ya Sabasaba 2025, msimu wa 49, ambayo ni muimili wa nchi za Afrika Mashariki. Maonesho ya Sabasaba yamebeba kauli mbiu inayosema, "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania".