Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KONGAMANO LA EGYPT NA TANZANIA KUIMARISHA BIASHARA

  • February 5, 2025

Tanzania na Egypt waendeleza ushirikiano wa kibiashara kwa kulenga kuimarisha uchumi baina ya nchi izo mbili, kupitia kongamano hilo fursa mbalimbali zimeweza kupatikana kwenye sekta za Ujenzi, Kemikali, Nishati, Kilimo, Vifaa vya Usafi wa majumbani Kongamano hili limefanyika leo tarehe 4 Februari 2025.



Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa M. Khamis ameshiriki kongamano hilo na kuwahakikishia wageni hao kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa uwekezajı na mlango wa biashara kwa Afrika nzima. Mkurugenzi Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau wa biashara kutoka Egypt kujiandikisha na kuja kushiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu kama Sabasaba yanayofanyika kila mwaka kuanzia tarehe 28 Juni mpaka 13 Julai 2025 katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.