Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

WANANCHI WANEEMEKA UZINDUZI WA MAONESHO YA KWANZA YA GULIO LINDI.

  • November 4, 2024

2, Novemba 2024
Lindi.


__

Mhe. Dkt Selemani Jafo Waziri wa Viwanda na Biashara, azindua rasmi maonesho ya kwanza ya Gulio mkoani Lindi. Gulio hilo umelenga kuleta uchechemuzi Kwa wazalishaji wa kilimo cha mwani, pamoja na bidhaa nyingine za kibiashara kama vile, ufuta, korosho nk. Waziri Jafo awaomba wafanya biashara wa Lindi kusimamia swala la masoko kimtandao Kwa kuzingatia ubora na kuongezwaji wa thamani kwenye bidhaa mbalimbali.

Aidha Wanalindi wamemuomba Waziri kuangalia namna ya Wanalindi kupata viwanda vya kuchakata mazao yanayolimwa Mkoani Lindi jambo likatalopelekea ukuwaji wa uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja na nchi kwa ujumla