Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

CHINA NA TANZANIA YAENDELEA KUIMARISHA MAENDELEO YA BIASHARA NCHINI

  • August 23, 2024

22/08/2024
Dar es salaam
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki katika Jukwaa la Maendeleo ya pamoja kati ya Tanzania na Nchi ya China lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  mgeni rasmi alikuwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Bi. Kezia Mlaki ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa M Khamis alibainisha kuwa TanTrade imeendelea kuimarisha maendeleo ya biashara baina ya nchi hizi kwa kutangaza bidhaa mbalimbali za Tanzania katika nchi ya China ambapo bidhaa hizo zimekuwa zikitafutiwa masoko nchini China. Pia amebainisha kuwa TanTrade imekuwa ikiandaa Maonesho ya kibiashara ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wafanyabiashara kutoka China kuja Tanzania mfano Maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ambayo kwa mwaka huu yamekutanisha zaidi ya makampuni 300 kutoka China.