SABASABA 2025, KIDIGITALI ZAIDI, KIINGILIO, NAEGESHO YA MAGARI KILA KITU KWA NJIA YA MTANDAO.
- June 26, 2025

26 JUNI 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). Bi Latifa M. Khamis amewatoa hofu Watanzania na wageni watakao kuja kutembelea Maonesho ya SABASABA 2025 hakutokua na foleni kwa maana viingilio na malipo ya maegesho ya magari yanafanyika kwa njia ya mtandao (online). Maonesho ya Sabasaba 2025 yanaanza rasmi tarehe 28 Juni 2025, meainisha hayo leo katika semina ya awali ya washiriki wa Maonesho iliyofanyika katika ukumbi wa Rashidi Mfaume Kawawa(Dome) katika kiwanja cha Maonesho Sabasaba.