Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

KLINIKI YA BIASHARA, MKOMBOZI KWA WAFANYA BIASHARA

  • October 17, 2024

Wadau kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika kliniki ya Biashara ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)kwenye maonesho ya Saba ya Tekinolojia ya Madini Geita, maonesho haya yameratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, leo tarehe 6 Oktoba 2024.

Kliniki ya Biashara ambayo ipo chini ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inalenga kutatua changamoto zote za Biashara za ndani ya Tanzania na nje ya mipaka ya Nchi, TanTrade inatoa rai kwa wajasiriamali, wazalishaji, wamiliki wa wiwanda kuja kutembelea kliniki hiyo ambayo inapatikana katika maonesho ya Saba ya Tekinolojia ya Madini Geita katika Viwanja vya EPZ Bombambili Geita.