KONGAMANO LA BIASHARA NA UCHUMI BAINA YA TANZANIA NA IRAN LAZAA MATUNDA.
- October 17, 2024

17, Oktoba 2024.
Kongamano la Biashara na Uchumi baina ya Tanzania na Iran ambalo limeratibiwa na kuandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), limeangazia kuwakutanisha wadau wa biashara kutoka pande zote mbili, ikiwa ni siku ya pili ya kongamano hilo wadau hao wameendelea kubadilishana mbinu mbalimbali za kibiashara, kuongeza mtandao wa masoko nk.
Kwenye picha (wakwanza Kushoto), ni Elibariki Emmanuel Chambua kutoka TanSpice Agri Ltd, kampuni ya vijana wazawa wa Kitanzania inayojihusisha na taarifa za masoko na wakulima ambao wameshiriki kongamano la biashara baina ya Tanzania na Iran, wamefanikiwa kufanya biashara pamoja na kampuni kutoka Iran Parsian Co. katika mkutano wa biashara kwa biashara ulioendelea leo katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo kiwanja cha Mwl. Nyerere maarufu kama (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, Tanzania.