Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

BARAZA LA WATUMISHI WA TANTRADE LAKETI KUJADILI MASWALA MBALIMBALI YAKIUTENDAJI.

  • June 18, 2025

14, JUNI 2025.


Baraza la watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wamekutana leo na kufanya kikao kazi kilichohusisha mazungumzo yenye tija katika kuboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo, sambamba na kuangazia maswala mbalimbali ya kiudendaji kwa maslahi mapana ya taifa.

Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mkutano wa Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.