BANANA ZORRO BALOZI WA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM SABASABA 2025
- June 18, 2025

3 Juni 2025
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade katika kutekeleza majukumu yake ya uratibu wa Maonesho imefikia makubaliano na msanii wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Banana Zoro kuwa Balozi Rasmi wa SABASABA 2025.
Akiongea wakati akimtambulisha balozi huyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade Bi Latifa M. Khamis amesema kuwa Balozi huyo mpya atakuwa na jukumu la kutangaza na kuhabarisha umma wa Tanzania na nchi nyingine kuhusu Maonesho ya Sabasaba 2025.