Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

MSANII NANDY ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA 2025.

  • July 13, 2025

12 JULAI, 2025.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Nandy ametembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa lengo la kujionea bidhaa na huduma mbalimbali zilizopo katika Maonesho ya Sabasaba. Aidha Nandy alipata wasaa wa kutembelea banda la Made in Tanzania ambalo kuweka bidhaa zinazozalishwa Tanzania tu. Maonesho ya Sabasaba 2025 yamebeba kauli mbiu inayosema "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA fahari ya Tanzania." Maonesho haya makubwa zaidi Afrika ameanza tarehe 28 Juni na kutamatika Julai 13, 2025.