Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

TanTrade Fostering Business

BALOZI KAGANDA AIPA MAUA YAKE TANTRADE KUITANGAZA BIASHARA KIMATAIFA.

  • August 28, 2025

27 Agosti, 2025.

Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. Kamishna Suzana Kaganda amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt. Latifa M Khamis  na  kupongeza  TanTrade kwa kuendelea kuipaisha Biashara ya Tanzania katika Masoko mbalimbali ya Kimataifa yakiwemo masoko ya nchini Zimbabwe. Mhe. Kaganda amesema hayo leo katika ofisi za TanTrade jijini Dar es salaam.

Aidha alibainisha kuwa,  Zimbabwe ina fursa nyingi za soko la Biashara kwa Mazao ya Biashara ya Tanzania ikiwemo Mchele, Kahawa, Korosho pamoja na Mavazi mbalimbali ya asili ikiwemo batiki pamoja na Mvinyo(wine). Hivyo, alimualika Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt. Latifa M. Khamis katika Maonesho mbalimbali yanayotarajiwa kufanyika katika nchi ya Zimbabwe.

Kwa upande wake  Dkt. Latifa M. Khamis alimuhakikishia, TanTrade itashiriki ipasavyo katika Maonesho ambayo yatafanyika katika nchi ya Zimbabwe kwa ajili ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa Tanzania.