Kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji wakuu wa taasisi za UMMA

Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa
Taasisi za Umma “CEOs Forum” imeandaa kikao kazi kitakachowakutanisha
Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma 249
kitakachofanyika Jijini Arusha katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Arusha - AICC kuanzia tarehe 19 Agosti, 2023 mpaka 21 Agosti, 2023.
Lengo la kikao kazi hiki ni kuwakumbusha washiriki wajibu na msingi wa dhamana waliyopewa na Serikali katika kusimamia utendaji wa Taasisi za Serikali. Mada zitakazotolewa katika kikao hiki zitasaidia katika kuongeza ufanisi wa watendaji wa katika kusimamia utendaji wa Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika wanayoyasimamia.