NENO LA UKARIBISHO
Ninayo furaha na heshima kubwa kuwakaribisha katika Tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa ajili ya kufahamu masuala mbalimbali yanayoihusu Taasisi yetu ikiwa ni pamoja na kuijua sheria iliyoanzisha Taasisi hii, majukumu yanayotekelezwa na Taasisi yetu, matukio mbalimbali ya ukuzaji Biashara yanayoratibiwa na kuandaliwa na Taasisi kama vile Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa, Misafara ya Kibaishara, Makongamano ya Kibiashara na mengine.
Tovuti yetu pia itakuonesha namna Taasisi yetu inavyotekeleza shughuli mbalimbali zinazosaidia ukuzaji wa diplomasia ya uchumi kwa kushirikiana na Balozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizo katika nchi mbalimbali duniani.
Ni matumaini yetu kuwa baada ya kutembelea tovuti yetu ya
www.tantrade.go.tz utakuwa umejifunza masuala mengi zaidi kuhusu uendelezaji na ukuzajia wa Biashara nchini. Pia, tembelea katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili kuendelea kupata taarifa muhimu zitakazoendelea kukupa uelewa wa Taasisi yetu.
Karibuni sana!