Historia ya TanTrade

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilianzishwa na Sheria ya Bunge Na. 4 ya mwaka 2009 na kuanza shughuli zake rasmi tarehe 3 Septemba, 2010 (GN Na 338). Uanzishwaji wake ulitokana na kufutwa kwa Sheria ya Bunge Na. 15 ya 1973 iliyoanzisha Bodi ya Biashara ya Ndani (BIT) na Sheria ya Bunge Na. 5 ya 1978 iliyoanzisha Bodi ya Biashara ya Nje (BET). TanTrade ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya udhibiti, utendaji, na ushauri wa kuendeleza na kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi.