Majukumu ya TanTrade
- Kuishauri Serikali kwenye masuala ya kuunda, kuendeleza, kusimamia na kutekeleza sera na mikakati ya biashara;
- Kudhibiti na kutangamanisha maendeleo ya soko la ndani ya nchi (Regulate and Integrate the Domestic Market);
- Kushirikiana na taasisi nyingine katika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma;
- Kuijengea uwezo jumuiya ya wafanyabiashara juu ya namna bora ya kusimamia shughuli za biashara ya ndani na ya nje;
- Kuanzisha, kutunza na kuendeleza kanzidata ya taarifa za biashara nchini;
- Kuandaa na kuratibu Maonesho ya biashara, misafara na mikutano ya wafanyabiashara;
- Kukuza mahusiano na mawasiliano miongoni mwa wafanyabiashara, kufanya utafiti wa Masoko, uhakiki wa mahitaji, uendelezaji wa bidhaa na kuzifanyazikubalike katika soko la ndani na nje;
- Ukusanyaji na usambazaji wa taarifa mbalimbali za biashara kupitia kwenye machapisho na vyombo vya habari;
- Kutoa ushauri kwa Serikali, taasisi au asasi juu ya kuweka mfumo wa kuendeleza biashara kwa ufanisi, Mbinu za kuratibu na kusimamia mfumo wa utoaji wa leseni za biashara;
- Kutekeleza sera zinazohusiana na soko la ndani na la kimataifa kwa bidhaa za Tanzania ;
- Kuweka na kusimamia utekelezaji wa mahusiano mazuri ya biashara ; na.
- Kutoa na Kusimamia Vibali vinavyotolewa na TanTrade kwa Maonesho ya Kimataifa yanayofanyika nchini.